Published On: Mon, Dec 3rd, 2018

HAYA NDIO MATUNDA YA VITA DHIDI YA UJANGILI

Share This
Tags

Vita dhidi ya Ujangili wa Tembo katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha imeanza kuzaa  matunda, kutokana na mikakati  mbalimbali inayoendelea kuwekwa na na kutekelezwa na  mamlaka zinazosimamia hifadhi hiyo kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo.

Imeelezwa kuwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha imezungukwa na vijiji 21 vinavyounganisha Tarafa ya Pawaga na Idodi ambavyo kwa ujumla vinashiriki katika mapambano dhidi ya vitendo vya Ujangili wa Tembo jambo linalochangia kupunguza matukio hayo na kufanya idadi ya wanyama hao kuonezeka.

Izumbe Msindai ni  Muhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha akizungumza na Clouds tv iliyotembelea  katika hifadhi hiyo amesema kwa sasa matukio ya ujangili yamepungua kutokana na jitihada zinazofanywa na Hifadhi kwa Kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi.

Pamoja na jitihada hizo za kupambana na  ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha lakini pia zipo  changamoto za uwindaji haramu, unaodaiwa kufanywa na  wawindaji wenye vitaru kwakutumia mbinu mpya  ya kuwa fukuzia wanyama hao nje ya hifadhi kwa kutumia ndege , vitendo  ambavyo vinadaiwa kuisababishia hasara  serikali kama anavyoeleza Meneja Ujirani Mwema TANAPA Ahmedi Mbugi.

Lakini je,wananchi wanazungumziaje jitihada hizo za kutokomeza vitendo vya ujangili? Huyu hapa ni Christopher Mademla na Noel Kalulu wakibainisha.

Pamoja na uwepo wa  changamoto a ujangili wa Tembo katika hifadhi za Taifa Kwa mujibu wa mfumo wa Ikolojia ya Ruaha Rungwa inataja kuwepo kwa wastani wa Tembo zaidi ya elfu 20 huku mikakati mbalimbali ya ulinzi kumuokoa mnyama huyo ikiboreshwa.

Shirika la msaada la Marekani (USAID) katika mradi wake wa protect kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari Tanzania Jet ndio wawezeshaji wa mradio huu wenye lengo la kuhakisha wandishi wa habari wanajikita kwenye uandishi wa habari za Uhifadhi wanyamapori na Utalii.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>