Published On: Wed, Oct 31st, 2018

WAANDISHI WA HABARI WAFUNZWA KUHUSU MAZINGIRA

Share This
Tags

Mabadiliko ya Tabia nchi duniani yanatanjwa kuwa tatizo sugu linalozikumba nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania nakuleta athari sektambalimbali ikiwemo ya wanyamapori.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani katika wa mafunzo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari  za Mazingira (JET) kwa ufadhiliwa wa Shirika la Misaada la Marakeni (USAID Protect), Mtaalamu wa masuala ya Maliasili  kutoka Shirika hilo Joseph Olila amesema mabadiliko ya tabia nchi ndio tatizo kubwa ambalo hadi sasa halijapatiwa ufumbuzi.

Ameongeza kuwa mabadiliko  ya tabia nchi yamekuwa yakiathiri kila sekta nchini ikiwemo masuala ya Uhifadhi wa  Wanyamapori  na Utalii hivyo ni wazi kwamba juhudi kubwa zinatakiwa kufanyanywa ili kunusuru janga hilo.

Akizungumza na Clouds Fm mapema Jana  Mkurugenzi Mtendaji wa JET John Chikomo amebainisha  lengo la mafunzo hayo kuwa ni kuhakikisha kuwa jamii na waandishi wa habari wanapata uelewa juu ya masuala yote ya wanyamapori ikiwemo sekta binafsi kutumia fursa ya kuwekeza katika sekta hiyo ya wanyamapori

Aidha ameongeza kuwa JET itandelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili kusaidia jamii pamoja na taifa kwa ujumla kuwa na uelewa juu ya uhiadhi wa mazingira.

Naye Mwanasheria kutoka Chama cha Wanasheria wa Mazingira (LEAT) Stanslaus  Nyembea amegusia sheria nyingi ikiwemo ya wanyamapori  kuwa bado zimekuwa na changamoto kubwa katika utekelezaji wake hali inayosababisha  migogoro katika hifadhi na wananchi.

Posted By

-

Displaying 1 Comments
Have Your Say
  1. Thanks! And thanks for sharing your great posts every week!generic cialis

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>