Published On: Wed, Aug 1st, 2018
World | Post by jerome

Zimbabwe yawaonya wagombea dhidi ya kutangaza matokeo

Share This
Tags

Serikali ya Zimbabwe imewaonya wagombea wa uchaguzi kuwa watashitakiwa na kufungwa jela kwa kutangaza mapema matokeo ya uchaguzi wa kihistoria baada ya chama cha upinzani Movement for Democratic Change – MDC kusema kuwa kimeshinda.

Waziri wa Mambo ya Ndani Obert Mpofu amesema serikali itawachukulia hatua za kisheria viongozi wa vyama wanaosema wazi kuwa watatangaza matokeo yao bila kuzingatia sheria.

Chama cha MDC kilidai kupata ushindi jana katika uchaguzi ambao Rais Emmerson Mnangagwa alisema unaonekana kumpa ushindi. Maafisa wa tume ya uchaguzi wamesema matokeo ya uchaguzi huo bado yako mbali sana na kuwa hakuna tangazo litakalotolewa kabla ya Jumamosi.

Afisa wa MDC Tendai Biti alisema kuwa wana uhakika kuwa mgombea wao Nelson Chamisa ameshinda na kama hatotangazwa mshindi, watayatangaza matokeo yao wenyewe.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>