Published On: Thu, Aug 16th, 2018

Waziri Mwakyembe kuzungumza na watendaji wakuu TRA

Share This
Tags

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewaahidi wadau wa sekta ya filamu  Mkoa wa Geita kufikisha  maombi yao ya kupatiwa stika za TRA kwa kazi zao kwa watendaji wakuu wa TRA iliwaweze kupatiwa stika hizo katika ofisi ya TRA za  mkoani hapo.

Mwakyembe ametoa ahadi hiyo leo mkoani Geita katika kikao na wadau wa kisekta wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ambapo kikao hicho kililenga  la kupata taarifa na kujua changamoto za wadau hao ili serikali iweze kuchukua hatua stahiki.

Akizungumza na wadau hao Waziri huyo alieleza kuwa serikali kupitia idara yake ya Sanaa inaangalia namna ya kutafuta wafadhili watakao toa ufadhili wa kulipia mafunzo ya huduma katika ndege ili washindi wa mashindano ya urembo waweze kupata kazi ya kutoa huduma katika  Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Pamoja na hayo Msemaji Mkuu wa Serikali Tanzania Dkt.Hassan Abbas alitoa elimu ya matumizi ya sheria mbili  ambazo ni Sheria ya Haki yakupata taarifa ya mwaka 2016 na Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016,ambapo sheria hizi zinazohusu sekta ya habari na kuwafafanulia waandishi wa habari mipaka yao katika mambo ya kuyatolea habari ikiwemo mambo yanayohusu usalama wa taifa.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alieleza kuwa ofisi ya mkoa inashuhughulikia suala la kupatikana kwa eneo la uwanja wa michezo utakao kuwa unatumika kwa ajili ya wanamichezo kufanyia mazoezi na mashindano kwa sasa wakati eneo lililotengwa kwa ajili ya kujengwa uwanja wa kimataifa likiendelea kufanyiwa mchakato wa kufanyiwa ujenzi.

Hata hivyo Mhe. Mwakyembe ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Geita kwa namna unavyotekeleza mikakati yake ya maendeleo na juhudi mbalimbali ambazo wamekisha zifanya katika kuubadilisha mkoa huo na kuwa wa kisasa zaidi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>