Published On: Mon, Aug 13th, 2018
World | Post by jerome

Watu 39 wauawa Idilib Syria

Share This
Tags

Kiasi ya watu 39 wameuawa jana Jumapili miongoni mwao watoto kufuatia mripuko uliotokea katika ghala la silaha katika kijiji cha Sarmada kilichopo katika jimbo la Idlib hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake nchini Uingereza.

Ghala hilo la silaha lilikuwa katika jengo la makazi ya watu na mripuko huo umesababisha majengo mawili kubomoka. Afisa wa wizara ya ulinzi nchini humo amelieleza shirika la habari la DPA kuwa waokoaji ikiwa ni pamoja na maafisa wa zima moto walikuwa bado wakiendelea kuwaondoa watu kutoka katika vifusi.

Vikosi vya serikali vimetoa wito kwa raia kuanza kuondoka kabla hawajaanza operesheni dhidi ya waasi katika eneo hilo ambao wengi wao wanahusishwa na kundi la itikadi kali la al-Qaeda.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>