Published On: Mon, Aug 13th, 2018

Wasaidizi wa kisheria wakwamishwa na mila na desturi za makabila.

Share This
Tags

Tatizo la Mila na Desturi za makabila mbalimbali nchini limeendelea kuonekana kuwa kikwazo kwa wananake kushindwa kupata fursa ya kudai haki zao kutokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kuendelea ikiwemo kukosa haki ya kumiliki ardhi na vipigo.

Wasaidizi wa kisheria ambao wamekua wakitoa huduma ya kuwapa wananchi msaada wa kisheria wamesema kutokana na mila na desturi za makabila mbalimbali nchini  wanawake wengi  wenye uhitaji wamekuwa wakishindwa kujitokeza kupata msaada.

Akizungumza jijini Dodoma mjumbe wa shirika la wasaidizi wa kisheria  [paraligos]  JOHN SHIJA amesema  wamekua wakipata wakati mgumu kuwafikia wanawake wa vijijini na kuwapa elimu ya msaada wa kisheria kwani wengine mila zao haziwaruhusu kwenda kwenye mikutano ya hadhara.

RAMADHANI MASELE ambaye ni meneja wa program kutoka shirika la legal services facility, amesema wamekutana Dodoma na wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria ili kuangalia namna ya kutatua changamoto za kuwafikia wanawake zaidi.

Kwa upande wa wizara ya katiba na sheria kupitia kwa msajili wa mashirika yanayotoa msaada wa kisheria bi FELISTA MUSHI  imewapongeza wasaidizi wa kisheria nchini ambao wamekua wakifanya kazi kubwa ya kuwasaidia wananchi kuzijua na kuzidai haki zao.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>