Published On: Thu, Aug 16th, 2018

Wanafunzi watoro wasakwa.

Share This
Tags

Serikali wilayani Muleba imeanza operesheni maalumu ya nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwasaka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, ambao waliacha masomo na kukimbilia visiwani kufanya shughuli za uvuvi ,vibarua majumbani na waliobebeshwa ujauzito na kufichwa na wazazi wao.

Operesheni hiyo maalumu inaongozwa na mkuu wa wilaya ya Muleba mhandisi Richard Ruyango, imewanasa jumla ya wanafunzi 9 wa kidato cha kwanza na cha pili wa shule ya  sekondari ya Kibanga, ambapo baadhi ya wanafunzi waliokamatwa  wameelezea kuwa wanalazimika kuacha masomo kutokana  na kuwa na uwezo mdogo madarasani.

Mhandisi Ruyango ametoa onyo kali kwa watendaji wa serikali za vitongoji  pamoja na wakuu wa shule wanaoshirikiana na watu  wanaowapachika mimba wanafunzi na kuahidi  kuwachukulia hatua kali wale wote watakaokamatwa kwa kuhusika na  vitendo hivyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>