Published On: Mon, Aug 13th, 2018
Business | Post by jerome

UberBoat: Kampuni ya Uber kuanzisha usafiri wa boti Tanzania

Share This
Tags

Kampuni ya huduma za usafiri inayotumia programu tumishi Uber imetangaza mpango wa kuanzisha huduma za boti Tanzania.

Kampuni hiyo kufikia sasa imekuwa ikitoa huduma za usafiri kupitia magari na bajaji.

Huduma hiyo mpya itafahamika kama UberBoat.

Meneja masoko wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki, Elizaberth Njeri amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema huduma zilizopo za Uber zimefanikiwa vyema na ndio maana wakaamua kuanzisha pia huduma ya boti.

Kadhalika, Dar es Salaam ni mji wa pwani pamoja na visiwa vya Zanzibar na hivyo usafiri wa boti utafaa sana.

“Dar es Salaam imezungukwa na fukwe nzuri na visiwa vidogo vidogo lakini watu hawapati ladha halisi ya mandhari hayo kwa kuwa hawajui wanawezaje kufika huko. Huduma ya Uberboat ambayo inakaribia kuanza hivi karibuni itasaidia hilo,” amesema Bi Njeri.

Hata hivyo, hakueleza ni lini huduma hiyo itaanza.

“Siwezi kusema ni lini hasa, lakini ni ‘very soon’ (hivi karibuni) inaweza ikawa wiki mbili zijazo au mwezi mmoja lakini ndo hivi tumekwisha zindua. Hatutaishia Dar es Salaam na Zanzibar tu, tunatarajia kwenda na maeneo mengine kulingana na uhitaji wa soko.”

Posted By

-

Displaying 5 Comments
Have Your Say
 1. Ecgklk says:

  buy essay now – write essays for money great essay writers

 2. Rhfzbd says:

  cheap essays online – write my thesis easy essay help

 3. Qpfbth says:

  buying an essay – letter editing essay writer funny

 4. Dcuqyx says:

  essays writing – order research paper help on essay

 5. Vyazfb says:

  cheap paper writing – essays online to buy essay writer website

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>