Published On: Tue, Aug 7th, 2018
Sports | Post by jerome

Thibaut Courtois na Willian: Mlinda lango wa Chelsea agomea mazoezi, atahamia Real Madrid? Willian alitafutwa na Barcelona

Share This
Tags

Mlinda lango wa ChelseaThibaut Courtois, ambaye amehusishwa na kuhamia Real Madrid, hakufika kwa kikao cha mazoezi katika klabu hiyo inayocheza Ligi Kuu ya England siku ya Jumatatu na wala hakutoa taarifa.

Inafahamika kwamba Chelsea hawajui ni lini Mbelgiji huyo mwenye miaka 26 atarejea.

Duru zinasema huenda akawa anataka kulazimisha uhamisho wa kwenda Real Madrid, klabu ya Uhispania ambayo imekuwa ikimtafuta kwa muda mrefu.

Courtois amekuwa mchezaji wa Blues tangu 2011, alipojiunga nao kutoka klabu ya Genk ya Uholanzi. Misimu ya kwanza alitumwa kwa mkopo Atletico Madrid nchini Uhispania.

Winga wa Chelsea Eden Hazard amehusishwa pia na Real, lakini hakuhudhuria pia mazoezi Jumatatu.

Courtois alitawazwa mlinda lango bora wa michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi ambapo Ubelgiji waliwazidi nguvu England na kumaliza wa tatu katika michuano hiyo.

Amechezea Chelsea mechi 154 na kumaliza mechi 58 bila kufungwa. Amefungwa jumla ya mechi 152.

Akiongea Ijumaa, meneja mpya wa Chelsea Maurizio Sarri alisema hana uhakika iwapo Courtois atasalia katika klabu hiyo.

“Kwa sasa Courtois ni kipa wa Chelsea. Sijui kuhusu siku zijazo. Inategemea klabu, lakini pia inamtegemea zaidi yeye binafsi, lakini natumai kwamba Courtois ataendelea kuwa golikipa wetu.”

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>