Published On: Thu, Aug 16th, 2018

Tanapa imezindua mpango bora wa matumizi ya ardhi.

Share This
Tags

Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA limezindua mpango wa matumizi bora ya Ardhi kwenye Vijiji vinavyozunguka Hifadhi zote nchini ambapo itaanza kwenye hifadhi tatu za kaskazini mwa nchi ambazo ni Hifadhi ya Tarangire,Manyara na Serengeti.

Mpango umekuja kutokana na kuongezeka kwa Migogoro ya ardhi.

Josephat Hasunga ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ameelezea hayo katika uzinduzi wa utekelezaji wa mpango wa matumizi ya ardhi ya vijiji 95 vinavyopakana na hifadhi za Taifa kwa lengo la kupunguza migogoro.

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi anasema sasa wizara yake haitafanya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji ambavyo tayari imeshavipangia kwa kuwa serikali inaingia gharama kubwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amasema migogoro ya Ardhi imekithiri  hasa kanda ya kaskazini na kurudisha nyuma maendeleo.

 

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>