Published On: Tue, Aug 14th, 2018

RC Hapi ataka kasi ya utoaji mikopo ya halmashauri iongezwe.

Share This
Tags

Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imetakiwa kuongeza kasi ya Utoaji wa Mikopo  kwa vikundi vya wanawake na vijana ambayo ni asilimia 10 inayotengwa kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri.

Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya kilolo ikiwa ni katika siku ya kwanza ya ziara yake katika halmashauri za mkoa huo ambapo amesema ni vema mikopo hiyo vikatolewa vitendea kazi badala ya fedha ili kumsaidia mwananchi katika usindikaji wa bidhaa mbalimbali.

Katika hatua nyingine Hapi ameitaka halmashauri hiyo kuongeza kasi ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato ili yaweze kusaidia katika kujenga miradi ya maendeleo itakayokuwa na tija kwa jamii.

Mkuu huyo wa Mkoa ameanza ziara ya siku tatu katika halmashauri za mkoa huo, akilenga kuzungumza na watumishi wa halmashauri na kutoa mwelekeo wa serikali katika kipindi chake kwa lengo la kuboresha utendaji na utoaji huduma kwa wananchi huku akihimiza uadilifu na umoja.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>