Published On: Tue, Aug 14th, 2018

Naibu waziri wa fedha akosa imani na meneja TRA Kigoma

Share This
Tags

Naibu waziri wa Fedha Dr Ashatu Kijaji, ameeleza kukosa imani na utendaji kazi wa Meneja wa Mamlaka ya Mapato TRA mkoani Kigoma, kwa kushindwa kusimamia suala la utoaji risiti wakati wa kuuza na kununua bidhaa kwa wafanyabiashara mjini Kigoma.

Amebainisha hilo katika kikao na wafanyabiashara mjini Kigoma, ambapo amedai kuwa utafiti mdogo alioufanya katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Kigoma, amegundua kuwa wafanyabiashara hawatoi risiti wakati wa kuuza na kununua bidhaa.

Naibu waziri huyo wa fedha amefika Kigoma kwa lengo la kuongea na wafanyabiashara ili kufahamu mazingira ya biashara yalivyo Kigoma, fursa zilizopo, pamoja na vikwazo vya kufanya biashara ikiwemo viwango vya kodi, ili kuangalia namna ya kuvipatia ufumbuzi.

Baadhi ya vikwazo vya kibiashara vilivyobainishwa ni pamoja na Dola 50 inayolipwa na wajasiriamali wenye mitaji midogo kwa ajili ya Viza ya kusafiria kupeleka bidhaa zao nchi jirani, ambayo wadau wameshauri iondolewe, na pia kikwazo kingine ni ukadiriaji wa kodi na lugha inayotumika kwenye fomu za kujisajili kama mlipa kodi.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>