Published On: Thu, Aug 16th, 2018

Mycoplasma Genitalium: Mambo muhimu kuhusu ugonjwa wa zinaa wa MGen unaokuwa sugu na kuzua wasiwasi duniani

Share This
Tags

Wataalamu maeneo mbalimbali duniani, wametoa tahadhari kuhusu ugonjwa mpya wa zinaa ambao unaonesha dalili za kutosikia dawa na kuzua wasiwasi sawa na ulioibuliwa na ugonjwa wa Ukimwi.

Ugonjwa huo unafahamika kitaalamu kama mycoplasma genitalium, na ufupisho wake kwa Kiingereza ni MGen na wakati mwingine umekuwa ukifupishwa tu kama MG.

Ugonjwa huo uligunduliwa miaka ya 1980 lakini ni miaka ya karibuni ambapo wanasayansi walibaini kwamba kuenea kwa ugonjwa huo kunahusiana na tendo la ndoa.

Bakteria za mycoplasma genitaliumhuambukiza seli zilizo kwenye mfumo wa mkojo na njia ya uzazi.

Hapa tumekuandaliwa mambo muhimu unayofaa kuyafahamu kuhusu ugonjwa huu kama yanavyosimuliwa na Dkt Suneeta Soni ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi nchini Uingereza na Dkt Pam Sonnenberg aliyewahi kuongoza utafiti kuhusu MGen.

Je, ugonjwa huu ni wa aina gani?

MGen ni ufupisho wa mycoplasma genitalium na ni ugonjwa ambao unaathiri wanaume na wanawake.

Nchini Uingereza inakadiriwa kwamba asilimia moja ya watu wote wameambukizwa ugonjwa huo.

Ugonjwa huo umeelezwa kama ugonjwa sugu usiosikia dawa ambao kuna hatari kwamba huenda ukafanikiwa kuhimili dawa zote na matibabu yote ambayo yapo kwa sasa.

Ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria kinyume na Ukimwi ambao husababishwa na virusi.

Bakteria za ugonjwa huu zimeonesha dalili za kuhimili antibiotiki ambazo awali zilikuwa zinatumiwa kuangamiza viini hivyo.

Viini vya ugonjwa huo viligunduliwa mara ya kwanza kwenye mfumo wa kupitisha mkojo wa binadamu mwaka 1981 katika hospitali ya St Mary’s, Paddington jijini London, na hatimaye vikatambuliwa kuwa vya jamii mpya ya viini ya Mycoplasma mwaka 1983.

Ni ugonjwa ambao umetambuliwa kama magonjwa ambao mara nyingi unaambatana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na unaathiri pia kwa kiwango cha juu kidogo wapenzi wa jinsia moja.

Wataalamu wanasema ugonjwa huo huenda ukachangia pia katika kuzuka kwa saratani ya tezi dume na saratani ya ovari katika baadhi ya watu.

Wanaougua ugonjwa huo wamekuwa wakitibiwa kwa antibiotiki za familia moja ambazo zinafahamika kama Macrolide ambapo ile maarufu ni dawa ya azithromycin. Kuna pia dawa nyingine kwa jina doxycycline. Bakteria za ugonjwa huo hata hivyo zinaanza kutosikia dawa hizo. Dawa ya azithromycin hata hivyo bado inafanikiwa kuwatibu baadhi ya watu ingawa madaktari wanalazimika kuongeza kipimo cha dawa mara nyingi.

Kiwango cha kutosikia dawa za Macrolide miongoni mwa bakteria za ugonjwa huo Uingereza kinakadiriwa kuwa asilimia 40 kwa sasa.

Dalili zake ni gani?

Dalili zake zinafanana sana na za ugonjwa mwingine unaofahamika kama chlamydia. Kwa wanaume, kuhisi maumivu wakati wa kupitisha mkojo na pia kutoa uzaha uumeni. Wanaume pia huhisi maumivu kwenye korodani.

Kwa wanawake, ni kuhisi maumivu kwenye sehemu ya chini ya tumbo na kwenye sehemu ya nyonga. Kadhalika, kuhisi maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa na pia baadhi wanaweza wakavuja damu kwenye sehemu nyeti.

Wanawake wanaweza pia kukumbwa na tatizo la mimba kukaa nje ya mji wa mimba.

Idadi kubwa ya watu walioambukizwa ugonjwa huu, karibu asilimia 90, huwa hawaoneshi dalili zozote, na kuna uwezekano kwamba miili yao itafanikiwa kuangamiza viini hivyo mwilini bila tiba yoyote na hivyo kwao hakuna haja ya kuwa na wasiwasi.

Unaweza kusababisha ugumba?

Madhara ya ugonjwa huu yanakaribiana sana na ya chlamydia; ambapo mwanamume huvimba na kuambukizwa kwa mirija ya uzazi na mji wa mimba pia.

Hilo linaweza kusababisha kuwepo kwa makovu na vidonda kwenye viungo hivyo jambo linaloweza kusababisha mwanamke baadaye kuwa gumba au tasa.

Unawezaje kujikinga na kujiepusha na ugonjwa huu?

Njia moja ni kujizuia kufanya mapenzi bila kinga. Hili litakukinga pia dhidi ya magonjwa mengine kadha ya zinaa.

Dkt Sonnenberg anasisitiza umuhimu wa kupunguza idadi ya watu ambao mtu anashiriki nao tendo la ndoa.

“Kadhalika, usifanye mapenzi na zaidi ya mpenzi mmoja kipindi kimoja kwani hivyo ndivyo ugonjwa unavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Madaktari wanapendekeza watu watumie mipira ya kondomu wanapofanya ngono na wapenzi wengine au wanapokuwa na wapenzi wengi.

Baadhi ya watu walio na dalili za ugonjwa huu wanaweza kutembelea hospitali au zahanati ambapo madaktari hawana uwezo wa kuupima ugonjwa huu.

Dkt Soni anasema hapo ndipo kuna tatizo kubwa katika kukabiliana na ugonjwa huo kwa sababu madaktari katika hali kama hiyo watakuwa wanatibu dalili badala ya ugonjwa wenyewe.

Kutokana na hilo, watu wengi wanaishia kupewa dawa za kukabiliana na bakteria (antibiotic) ilhali ukweli ni kwamba katika kipindi hicho wanakuwa hawazihitaji.

Hilo linachangia aste aste bakteria zinazosababisha MGen kuanza kuwa sugu na kuzoea dawa hizo.

Dkt Peter Greenhouse, mshauri wa masuala ya ngono huko Bristol anawashauri watu kuchukua tahadhari zaidi.

“Ni wakati ambapo watu wanafahamu kuhusu Mycoplasma genitalium,” alisema.

“Kuna sababu nzuri ya kubeba kondomu wakati wa likizo za msimu wa joto na kuzitumia.

Posted By

-

Displaying 6 Comments
Have Your Say
 1. Ismiha says:

  write papers online – help writing papers essay online help

 2. Grymgj says:

  how to write my thesis – help writing essays best writing service

 3. Jathho says:

  essay edit – help writing research paper buying an essay

 4. Ydzksj says:

  essays for sale online – assignments for sale write my essay

 5. Vdrrzq says:

  cialis online cheap https://saleciatad.com/ buy cialis on line Kzflci nybswa

 6. Qbbutn says:

  cialis for sale https://oktadalaf.com/ canada drugs online reviews Kjdbkp jamzyt

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>