Published On: Mon, Aug 13th, 2018

Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe ajiunga na CCM

Share This
Tags

Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA Mkoa wa Njombe Fackii Lulandala na makada wengine watatu wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, wamejivua uanachama na kujiunga na chama cha mapinduzi kwa madai ya kuridhishwa na utendaji wa serikali iliyopo madarakani.

Makada wengine ambao wameambatana na mwenyekiti huyo ni Edger Msigwa,Lukasi Payovela na Paulo Zakaria ambao wanasema wamechukua maamuzi ya kurejea chama tawala walikokuwa awali baada ya kuona mambo mengi yaliokuwa yakipigiwa kelele na vyama vya upinzani yanatekelezwa na serikali ya Dr Magufuli.

Wakizungumza katika mkutano na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa kadi za ccm, makada hao wa chadema wamekanusha kuhusu suala la kununuliwa kama ambavyo linazungumzwa na wapinzani zaidi ya kuridhishwa na mwenendo wa kiutendaji wa serikali Iliyopo madarakani .

Kwa upande wake katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpagike na Erasto Ngole ambae ni katibu mwenezi mkoani humo, wanasema jamii za watu wa Njombe zitegemee kuona makada wengi wa upinzani wakijiunga na chama cha mapinduzi kwa kuwa chama hicho kimejipambanua kuwapigania watanzania.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>