Published On: Tue, Aug 7th, 2018
Sports | Post by jerome

Mpira wa Kikapu, Rwanda: Rais Kagame aongoza uzinduzi wa mafunzo ya NBA kwa vijana

Share This
Tags

Rais wa Rwanda Paul Kagame, jana ameongoza shughuli za uzinduzi wa kambi maalum ya mafunzo kwa ajili ya kuibua vipaji vya mchezo wa mpira wa kikapu barani Afrika, iitwayo Giants of Africa, zilizofanyika katika uwanja wa mpira wa kikapu ulioboreshwa wa Nyamirambo.

Program hiyo ya kila mwaka ambayo ni pendekezo la chama cha mpira wa kikapu cha Marekani NBA, ilizunduliwa rasmi mwaka 2015, na kwa mwaka huu nchini Rwanda inafanyika kwa siku tatu kuanzia jana hadi jumatano, ambapo zaidi ya vijana hamsini watanolewa vipaji vyao, na baadhi ya makocha kutoka Rwanda watabadilishana mbinu na makocha wazoefu wa mchezo huo kutoka NBA.

Katika uzinduzi huo, Rais Kagame aliungana na Waziri wa michezo wa Rwanda Bi Julienne Uwacu, kiongozi mkuu wa NBA Adam Silver, Rais wa timu ya Toronto Raptors ya ligi kuu Marekani Masai Ujiri, pamoja na Amadou Gallo Fall ambaye ni makamu wa Rais wa NBA na Mkurugenzi wa tawi la NBA barani Afrika, ambapo pamoja na shukrani alizotoa kwa NBA, Rais Kagame aliwasifu vijana waliojitokeza na kuwahimiza suala la kutimiza ndoto zao.

Mbali na Rwanda, Giants of Africa inaendesha mafunzo hayo katika nchi za Nigeria, Kenya, Ghana, DRC, Senegal na Ivory Coast.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>