Published On: Tue, Aug 14th, 2018
World | Post by jerome

Korea Kusini na Kaskazini kuwa na mkutano wa kilele Septemba

Share This
Tags

Korea Kaskazini na Korea Kusini jana zimetangaza zimefikia makubaliano kwa ajili ya mkutano wa kilele utakaozishirikisha nchi hizo mbili utakaofanyika mwezi ujao katika mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang.

Huo utakuwa mkutano wa tatu kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in . Maafisa wa pande zote mbili walifikia makubaliano hayo walipokutana katika mji wa mpakani wa Panmunjom.

Wakati tarehe wala agenda ya mkutano huo ikiwa bado haijapangwa viongozi wa nchi hozo mbili huenda wakajali masuala ya amani na uwezekano wa kuanzisha ushirikiano katika masuala ya uchumi pamoja na miradi mingine ambayo itaanza kutekelezwa pale vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini vitakapo ondolewa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>