Published On: Thu, Aug 16th, 2018
Sports | Post by jerome

Kevin de Bruyne: Kiungo wa Man City aumia akifanya mazoezi

Share This
Tags

Nyota wa Manchester City Kevin de Bruyne anachunguzwa zaidi kwenye goti lake la kulia baada ya kuumia akishiriki mazoezi Jumatano.

Ubaya wa jeraha hilo la kiungo huyo wa kati haujabainika kufikia sasa.

Mwaka 2016, alikosa mechi 12 baada ya kuumia goti lake la kulia wakati wa mechi ya nusufainali Kombe la EFL ambapo walipata ushindi dhidi ya Everton.

De Bruyne, 27, alitawazwa mchezaji bora wa msimu wa Manchester City msimu uliopita baada ya kuwafungia mabao 12 na kusaidia ufungaji wa mabao mengine 21.

Aliwasaidia City kushinda taji la Ligi ya Premia na Kombe la EFL.

City, walioanza kutetea taji lao kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal wamepangiwa kukutana na Huddersfield nyumbani kwao Jumapili.

Baadaye watacheza ugenini dhidi ya Wolves na kisha nyumbani dhidi ya Newcastle kabla ya mapumziko ya kimataifa.

Mechi yao ya tano ya msimu itakuwa nyumbani dhidi ya Fulham mnamo 15 Septemba kabla ya mechi yao ya kwanza hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 18 au 19 Septemba.

City walivunja rekodi kadha msimu wa 2017-18, ikiwa ni pamoja na kufikisha alama 100, na pia kushinda mechi 32 na kufunga magoli 106 msimu mmoja enzi ya Ligi ya Premia.

Akiongea na BBC katika mahojiano ya kina mabayo yatapeperushwa na BBC Jumamosi, De Bruyne anasema kwamba anaamini City hawatakuwa na msimu mzuri kama msimu uliopita hivi karibuni.

City wanjaaribu kuwa klabu ya kwanza kufanikiwa kutetea taji la Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza tangu 2009.

Baada ya City kuchapisha taarifa za kuumia kwa Mbelgiji huyo, mchezaji huyo alionekana akiwa amefungwa kitambaa cha kukaza goti na akitembea kwa kutumia kigongo wakati wa kuanza kuonyeshwa kwa makala ya Amazon ambayo inafuatilia maisha ya klabu hiyo katika msimu uliopita.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>