Published On: Tue, Aug 14th, 2018

Ilikuwaje Mtatiro akabadilika na kuwa kada wa CCM?

Share This
Tags

Maswali mengi yamezuka mara baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro ,kujivua uanachama wake na kuhamia chama tawala cha CCM.

Mtatiro ni mwanasiasa ambaye pia ni mchambuzi wa siasa na amekuwa akiandika makala nyingi kuikosoa serikali lakini sasa amehamia huko ambako amekuwa akikukosoa kwa muda mrefu.

“Nimejiridhisha kwa hitaji la nafsi yangu kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM” Julius Mtatiro aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari siku ya jumamosi,Agosti 11.

Mkurugenzi wa habari wa chama cha CUF,Abdul Kambaya amesema zaidi ya asilimia 70 ya migogoro ya chama hicho imesababishwa na Mtatiro.

Chama hicho ambacho kimegawanyika katika pande mbili,kuna wale ambao ni wafuasi wa Profesa Ibrahim Lipumba na wale ambao wako chini ya Maalim Seif.

Awali chanzo cha migogoro ya ndani ya chama cha CUF ilidaiwa kuwa ni Profesa Lipumba kutangaza kutengua barua yake ya kujiuzulu nafasi ya uenyekiti aliyoiandika Agosti 2015, wakati wa kuelekea kwenye Uchaguzi mkuu.

Lakini kwa sasa mgawanyiko wa chama hicho umedaiwa kusababishwa na Julius Mtatiro kutokana na tabia zake za kibabe za kutotaka kusikiliza watu wengine.

Inakumbukwa kwamba mwanzoni mwa mwezi Julai,Mtatiro alikamatwa na polisi kutokana na ujumbe alioandika katika mtandao wa kijamii unaomkejeli rais John Magufuli kwa kusema kuwa ‘rais kitu gani?’

Aidha kujiengua kwa mwanasiasa huyo kumepelekea baadhi ya watumiaji wa mtandao wa kijamii kuanzisha kampeni za kuonesha kupinga au kukasirishwa na uamuzi wake kwa kuwataka watu waache kumfuatila kwenye mitandao ya kijamii kutokana na uamuzi wake kuonekana kuwa wa kisaliti.

Lakini vilevile Mtatiro alikuwa ni kiongozi wa upinzani ambaye alikuwa anawabeza wanasiasa wengine kuhamia CCM lakini sasa yeye ndiye ameamua kuhamia CCM.

Pamoja na kwamba Julius Mtatiro alifahamika kuwa mwanachama wa CUF,ila mwezi julai mwaka huu jumuiya ya vijana za CUF(JuviCUF) ilimtaka Mtatiro kukaa mbali na chama hicho na kuacha tabia ya kuwashambulia viongozi wa juu wa chama cha CUF kupitia mitandao ya kijamii kwa kuwa wao hawamtambui kuwa mwanachama wa chama hicho na aache tabia ya kupotosha umma.

Hatimaye sasa kile ambacho chama cha vijana CUF walichokuwa wanakihofia kuwa mwanasiasa huyo sio mwenzao kimeweza kudhihirika wazi.

Mtatiro aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF alitangaza kuhamia CCM siku ya jumamosi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>