Published On: Tue, Aug 14th, 2018
World | Post by jerome

HRW yataka uchunguzi ufanyike dhidi ya mauaji ya Misri mwaka 2013

Share This
Tags

Shirika la kimataifa la kutetea haki binadamu la Human Rights Watch limetaka kufanyika uchunguzi dhidi ya mauaji ya watu wengi waliouawa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya amani yaliyofanyika nchini Misri August 14,2013.

Mauaji hayo yalifanyika mjini Cairo wakati maelfu ya watu walipoandamana kupinga kuondolewa madarakani kwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo Mohamed morsi.

Kwa mujibu wa Human Rights Watch hadi sasa hakuna hata afisa mmoja wa vikosi vya usalama aliyeshitakiwa kwa kuhusika na mauaji hayo ambapo zaidi ya waandamanaji 800 waliuawa huku Misri ikichukua hatua kuwalinda maafisa wa kijeshi kutoshitakiwa.

Mwezi uliopita rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi aliidhinisha sheria inayotoa upendeleo kwa maafisa wa ngazi ya juu kijeshi pamoja na kuwapa kinga ya kidiplomasia wanaposafari nje ya nchi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>