Published On: Mon, Aug 13th, 2018

Biteko atoa wiki moja kwa mwekezaji kulipa kodi ya madini serikalini

Share This
Tags

Serikali imempa muda wa wiki moja mwekezaji mmiliki wa kampuni ya Amazon Trading (T) Company Limited Abdi Hozza kuhakikisha anailipa serikali kodi ya pango ya uwekezaji kiasi cha dola za Marekani  70,020 sawa na zaidi ya shilingi milioni 140 za kitanzania  anazodaiwa tangu mwaka 2011 katika machimbo ya Kalalani eneo la Umba wilayani Korogwe.

Sambamba na hilo imeiagiza serikali ya wilaya ya Korogwe  kuhakikisha inatenga maeneo ya wachimbaji wadogo wa madini ili kuepusha migogoro iliyodumu kwa muda mrefu hali ambayo imeleta chuki baina ya mwekezaji na wananchi.

Waziri Biteko alitoa agizo hilo alipotembelea katika machimbo hayo juzi Jumamosi katika vijiji vya Kigwasi na Kalalani kata ya Kalalani wilayani humo.

Awali diwani wa kata hiyo Amati Ngerera alimueleza naibu waziri kuwa mwekezaji huyo (Amazon) hana mahusiano mazuri na wanakijiji pamoja na wachimbaji wadogowadogo wa eneo hilo.

Amesema kuwa wananchi waliokuwa wakiingia eneo hilo walifanyiwa vitendo visivyokuwa vya kibinadamu ikiwemo kupigwa risasi na kubakwa na askari aliowaweka kulinda eneo hilo.

Diwani huyo alikwenda mbali zaidi kuwa mwekezaji huyo huwa anatumia eneo hilo kama dhamana ya kukopa fedha kutoka kwenye taasisi za fedha na alimpa mwenzake anaitwa Najim  kuendesha mgodi huo kinyemela bila ya serikali kuwa na taarifa.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigwasi, Loronyotu Lakaney alimueleza Naibu Waziri kuwa mbali na mgodi huo kutelekezwa na mwekezaji huyo pia madini yanatoroshwa kwa njia za panya na  kuuzwa Voi nchini Kenya.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>