Published On: Thu, Aug 16th, 2018
Business | Post by jerome

Bei ya jumla ya maharage imeshuka katika mikoa mingi nchini Tanzania.

Share This
Tags

Haya ni kwa mujibu wa Ripoti mpya ya kila wiki iliyotolewa na Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji ambayo imeonesha kuwa bei ya jumla ya maharage imeshuka katika mikoa mingi kwa wastani wa asilimia 30 ,kutokana na mavuno mazuri.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa mkoa wa Arusha umeandikisha bei ya chini zaidi ya maharage ambapo gunia la kilo 100 liliuzwa kati ya Sh90,000 na 150,000 tarehe 10 Agosti,bei ya chini zaidi kuliko wastani wa kati ya Sh125,000 na 170,000 tarehe 11 Mei mwaka huu.

Jijini Dar es Salaam bei ya maharage ni kati ya Sh170,000 na 200,000 kuanzia tarehe 10 Agosti,bei ya chini kuliko wastani wa Sh220,000 na 230,000 mwezi Mei mwaka huu.

Uchunguzi umebaini kuwa bei za rejareja za bidhaa hiyo jijini Dar es Salaam zimepungua hadi Sh1,800 na Sh2,300 kutoka bei ya Sh2300 na Sh2800 mwezi Mei mwaka huu.

Posted By

-

Displaying 1 Comments
Have Your Say
  1. Thanks! And thanks for sharing your great posts every week!viagra online

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>