Published On: Wed, Aug 1st, 2018

Agizo la waziri mkuu kuhusu michikichi laanza kutekelezwa

Share This
Tags

Siku chache baada ya eneo la Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Kihinga mkoani Kigoma, kupendekezwa kuwa eneo kitakapojengwa kituo cha utafiti wa zao la michikichi kama sehemu ya mpango wa serikali kufufua na kuendeleza zao hilo, Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba na watafiti wametembelea eneo hilo.

Jumamosi iliyopita katika kikao cha wadau wa zao la michikichi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,alibariki kujengwa kwa kituo cha utafiti katika eneo hilo na kuagiza mchakato wa ujenzi wa kituo hicho kuanza ikiwa ni pamoja kumuagiza Naibu waziri wa kilimo pamoja na wataalam wa utafiti kwenda kuangalia eneo hilo.

Tayari Naibu waziri ametekeleza agizo hilo kwa kutembelea na kukagua eneo hilo ambapo amebaini kuwa chuo hicho hakijafungwa kama ilivyoelezwa awali lakini akasema kuwa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 922 linatosha kuwa na kituo cha utafiti, na wakati huo huo chuo cha maendeleo ya jamii pia kikaendelea na shughuli zake.

Mkurugenzi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, NARI, Dr. Geoffrey Mkamilo, ameeleza kuridhishwa na eneo hilo na kusema kuwa uwepo wa kituo hicho utatoa fursa kwa wananchi kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu kilimo, huku Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, akieleza kuwa tayari halmashauri zimeagizwa kupeleka wataalam kupatiwa mafunzo maalum.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>