Published On: Wed, Aug 1st, 2018
World | Post by jerome

Afrika Kusini kufanya mabadiliko ya katiba kuhusu mageuzi ya mashamba

Share This
Tags

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema chama chake tawala cha African National Congress – ANC, kitawasilisha pendekezo la kuibadilisha katiba ili kuharakisha ugawaji upya wa mashamba kwa raia weusi wasio na mashamba ambao ndio wengi nchini humo.

Katika hotuba ya televisheni, Ramaphosa amesema chama chake kinakamilisha mchakato wa mabadiliko hayo ya katiba ambayo yanaeleza wazi mazingira ya kutwaliwa mashamba bila kutoa fidia.

Amesema hatua hiyo itachochea ukuaji wa uchumi. Idadi kubwa ya mashamba nchini Afrika Kusini bado inamilikiwa na wazungu, ikiwa ni miaka 24 baada ya kumalizika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi ambayo taratibu iliwanyima haki watu weusi na kuwaacha wakiwa masikini.

Wakulima wa kizungu wanadhibiti asilimia 73 ya maeneo ya kilimo na inaaminika kuwa ndio ardhi itakayotwaliwa kwa nguvu na kupewa watu waliokuwa wakiimiliki zamani ambao sasa ni maskini.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>