Published On: Tue, Jul 10th, 2018

Watendaji wasiowajibika wachukuliwe hatua-Ras Kigoma

Share This
Tags

Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, imeagizwa kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria watendaji wote watakaobainika kuhusika na vitendo vya ubadhirifu na kutowajibika ipasavyo na kwamba uchukuaji huo wa hatua ulenge watumishi katika ngazi zote.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Moses Msuluzya, katika mkutano wa baraza la madiwani kupitia taarifa ya CAG mwaka 2016/2017, ambayo ilibainisha mapungufu kadhaa ya kiutendaji ikiwemo suala la kutojibu hoja za mkaguzi mkuu wa serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Roja Lutobora Ng’olo, amesema agizo hilo tayari limeanza kufanyiwa kazi na ofisi yake kwa hatua ya awali ya kuwaandikia barua za karipio wote wanaohusika, na wale ambao wanastahili adhabu hatua zitachukuliwa katika kipindi cha siku 14 zijazo.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, amewapongeza wananchi na watendaji wake kwa kuiwezesha halmashauri hiyo kuongeza mapato kwa zaidi ya asilimia 30% ambapo katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai mwaka jana hadi Mei mwaka huu, halmashauri imekusanya shilingi bilioni 1.6, kutokana na vyanzo vya ndani.

Amesema kuongezeka kwa mapato kumechangiwa na halmashauri kuongeza vyanzo vya mapato pamoja na kuimarisha usimamizi na kwamba ongezeko hilo limesaidia kupunguza tatizo la vyumba vya madarasa ambapo kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita jumla ya vyumba 53 vimejengwa

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>