Wanawake kukuza utalii wa ndani Tanzania
Wanawake katika Utalii Tanzania (AWOTTA) wameshirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Tanzania (TWCC) kuanzisha maonyesho ya utalii ili kupiga jeki utalii wa ndani.
Hatua mpya ya kukuza utalii wa ndani, kwa kuzingatia juhudi za serikali katika kukuza ukuaji wa uchumi na kujenga nafasi za ajira
Mwenyekiti wa TWCC, Jackline Maleko amesema, kukuza utalii wa ndani na kutambua vivutio vipya ni wajibu wa kila mtu, amewahimiza, Watanzania katika maeneo yao kuwa wabunifu kwa kutambua vivutio ndani ya mazingira yao na kuitumia.