Published On: Tue, Jul 10th, 2018

Wananchi Serengeti wawajengea nyumba askari polisi kuimarisha usalama.

Share This
Tags

Wananchi wa Kijiji cha Rubanda Wilayani Serengeti Mkoani Mara wamewajengea nyumba za kuishi Askari Polisi waliopo katika eneo lao kutokana na ushirikiano uliopo huku wengine wakimuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kuwaongezea magari ya Polisi katika Wilaya hiyo kutokana na miundombinu yake jambo ambalo litawawezesha kuzuia uhalifu kabla haujatokea.

Wananchi hao wameyasema hayo wakati wa Ziara ya IGP Sirro inayoendelea katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzipatia ufumbuzi wa haraka ili wananchi waendelee kufanya kazi zao kwa Amani na utulivu.

Kwa Upande wake IGP amekubaliana na ombi hilo pamoja na kutoa tathmini fupi ya hali ya usalama hapa nchini ambapo amesema inaendelea kuwa shwari.

Katika hatua nyingine  IGP Sirro ametoa ushauri kwa Wakazi wa Kijiji hicho kusomesha watoto wao ili wasiwe tegemezi na kujiingiza katika vitendo vya kihalifu.

IGP anaendelea na ziara yake huku akitumia usafiri wa Helkopta ili kujionea kwa uhalisia maeneo hayo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto za uhalifu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>