Published On: Tue, Jul 10th, 2018

Uvivu kisababishi cha umaskini Kagera

Share This
Tags

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Mustapha Salum Kijuu amewataka watendaji wa serikali kuendelea kuwaelimisha na kuwahimiza wananchi kujikita katika kilimo na shughuli nyingine za uzalishaji  kwa kutumia ardhi na rasilimali zinazopatikana katika mkoa huo ili kuweza kuondokana na umaskini unaodaiwa kuukabili mkoa huo wa Kagera.

Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera ameseyasema hayo baada ya kupokea ripoti ya utafiti iliyofanywa na taasisi ya REPOA na kubaini viashiria vya umasikini katika wilaya ya Biharamulo,ambapo amesema hali hii inachangiwa na uvivu wa baadhi ya watu wanaoshindwa kutumia rasilimali zilizopo ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake mtafiti mwandamizi Dr.Blandina Kilama kutoka REPOA  ambaye amewasilisha ripoti hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Kagera, amesema utafiti ambao ulifanyika mwaka 2011 na  katika mkoa wa Kagera umebaini wilaya ya biharamulo ina viashiria vingi vya umaskini  mojawapo ikiwa ni lishe duni kwa watoto.

Kwa upande wao baadhi ya wadau walioshiriki katika uwasilishaji wa ripoti hiyo wakaeleza namna ya kuweza kukwamua mkoa huo ili uweze kusonga mbele kimaendeleo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>