Published On: Tue, Jul 10th, 2018
Business | Post by jerome

Tanzania inalitumia soko la Oman kwa kiasi kidogo sana kuuza bidhaa ndani ya nchi hiyo

Share This
Tags

Licha ya Nchi ya  Oman kuagiza bidhaa nyingi  Zaidi za  chakula kutoka nchi za nje, bado Tanzania inalitumia soko la Oman kwa kiasi kidogo sana  kuuza bidhaa ndani ya nchi hio.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo, naibu katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje na  africa mashariki balozi RAMADHANI MWINYI amesema kongamano hilo ni muhimu hasa kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawajalitumia vyema soko lililopo nchini Oman, kuuza bidhaa zao  kutokana na nchi hiyo kuhitaji bidhaa nyingi kutoka nje kunakosababishwa  na hali yake ya uzalishaji nchini OMAN.

Kuhusiana na bidhaa zinazohitajika ncini Oman, balozi wa Tanzania nchini humo ABDALA KILIMA amewataka watanzania kujitokeza kufanyabiashara OMAN, hasa za chakula huku akiwahimiza kuzingatia ubora wa bidhaa zao pamoja na kuzingatia ufungshaji.

Ujumbe huo wa wafanyabiashara wa Oman ni matokeo ya ziara aliyoifanya Rais mstaafu JAKAYA KIKWETE  nchini Oman alipokuwa Raisi ambapo kiongozi wa msafara huo, Mwenyekiti wa baraza la wafanyabiashara  nchini OMAN SAUD AL RAWADH amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kufanyabiashara OMAN huku akisisitiza kuwa baraza lake litatoa msaada wa kila aina ili kuhakikisha kuwa watanzania wanafanya biashara na Oman bila vikwazo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>