Published On: Wed, Jul 4th, 2018
Business | Post by jerome

Shirika la Reli Tanzania lafungua biashara Uganda

Share This
Tags

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limepania kurahisisha usafirishaji wa mizigo katika ukanda wa Afrika Mashariki na nchi nyingine za karibu.

Wiki iliyopita TRC ilirejesha safari za treni za mizigo kutoka Tanzania mpaka Kampala Uganda kupitia Tabora, Isaka, Mwanza na Ziwa Victoria kwa kutumia bandari ya Mwanza na Port Bell nchini Uganda.

Hatua hiyo imefanyika baada ya kusitishwa kwa usafiri huo kwa miaka 10, jambo ambalo kurejeshwa kwake kutaleta manufaa ya kiuchumi kwa nchi hizo mbali na wananchi wake.

Urejeshwaji wa safari hiyo, unaendeleza nyingine za wateja wao wakubwa ambao ni Burundi na Jamhuri ya Kidemokarasia ya Kongo (DRC) huku wakiwa na mipango ya kufufua njia za kupeleka mizigo katika nchi za Kenya na Rwanda ambako kwa sasa mizigo imeshuka.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>