Published On: Tue, Jul 10th, 2018
World | Post by jerome

Serikali ya Uingereza yatumbukia katika mgogoro

Share This
Tags

Mgogoro uliendelea kutokota katika serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, baada ya Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni Boris Johnson kujiuzulu, na kujiunga na waziri anayehusika na masuala ya Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya – Brexit, David Davis na naibu wake ambao walijiuzulu wakipinga mapendekezo ya May kuhusu mchakato wa Brexit.

Johnson alisema alijiuzulu kwa sababu hangeweza kukubali mpango mpya wa May wa kutaka kuendeleza mahusiano ya karibu na Umoja wa Ulaya baada ya Brexit na kwamba anahofia kuwa ndoto ya Brexit inakufa.

Nafasi yake imechukuliwa na Jeremy Hunt, waziri wa afya aliyehudumu kwa muda mrefu na ambaye ni mbunge wa chama cha Conservative na anayeonekana kuwa na mawazo sawa na ya Waziri Mkuu kuhusu Brexit.

Aidha May alimteua Dominic Raab kuwa waziri mpya wa masuala ya Brexit kuchukua nafasi iliyoachwa na David Davis.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>