Published On: Wed, Jul 4th, 2018
Sports | Post by jerome

Mbio za Baiskeli, Ufaransa: Uwizeye kutoka Rwanda ashinda ubingwa

Share This
Tags

Mwendesha baiskeli wa kimataifa wa Rwanda, Jean Claude Uwizeye ameshinda ubingwa wa mbio za kimataifa za siku za Ufaransa, ambapo aliandika rekodi ya kutumia saa 3, dakika 39 kwenye umbali wa kilomita 154.

Mshindi wa pili katika mbio hizo alikuwa Mael Boivin kutoka Canada aliyetumia saa 3, dakika 39 na sekunde 29, na mshindi wa tatu alikuwa Ben Carman kwa kutumia saa 3 dakika 39 na sekunde 38.

Huu ni ushindi wa pili kwa Uwizeye tangu ajiunge na klabu ya mchezo wa mbio za baiskeli Pays Olone CCL ya Ufaransa, kwani mwezi Mei pia alishinda mbio zingine za Ufaransa za Deauville Grand Prix.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>