Published On: Thu, Jul 26th, 2018
Sports | Post by jerome

Man City 1-2 Liverpool: Mohamed Salah na Sadio Mane waifungia timu yao

Share This
Tags

Mohamed Salah hakupoteza wakati wowote katika ufungaji wa mabao baada ya Liverpool kutoka nyuma na kuishinda Manchester City 2-1 mjini New Jersy Marekani.

Mshambuliaji huyo wa Misri , ambaye alifunga mabao 44 katika mechi 52 msimu uliopita alisawazisha bao lililofungwa na Leroy Sane katika kipindi cha pili dakika moja baada ya kuingia kama nguvu mpya mbele ya umati wa mashabiki 52,000.

Kichwa chengine cha Salah kilipanguliwa na kugonga chuma cha goli

Bao la penalti la Sadio Mane liliihakilkishia Liverpool ushindi wa kombe la kimataifa.

Salah na mshambuliaji wa Senegal Mane walikuwa wanacheza kwa mara ya kwanza tangu mataifa yao kuondolewa katika kombe la dunia katika awamu ya muondoano.

Bernado Silva wa Manchester City ambaye timu yake ya Ureno iliondolewa katika mechi ya kufuzu kwa robo fainali alicheza kwa mara ya kwanza, lakini City bado walikosa huduma za wachezaji 15 walioshiriki katika kombe la dunia Urusi.

”Ni kitu kizuri tulichofanya dhidi ya Liverpool waliotinga fainali ya kombe la vilabu bingwa katika dakika 75”, alisema kocha Pep Guardiola baada ya mechi hiyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>