Published On: Tue, Jul 31st, 2018

Julius Kalanga Laizer: Mwanasiasa mwingine wa upinzani ahamia CCM

Share This
Tags

Mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Julius Kalanga Laizer amejiuzulu na kujiunga na CCM kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Mbunge huyo amepokelewa na Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Humphrey Polepole huku akiwataka wapiga kura wake kumuelewa na kuahidi kuzungumza nao.

Kitendo cha wanasiasa kuhama vyama imekuwa si jambo geni Tanzania kwani siku chache zilizopita, mwanasiasa wa upinzani, Mwita Waitara alitangaza kujiengua katika chama kikuu cha upinzani cha chadema na kujiunga na Chama tawala, CCM.

Waitara aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga lililopo Dar es salaam alikishutumu chama cha Chadema, kuwa hakina demokrasia pia kutokuwa na maelewano na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Ikumbukwe kuwa wabunge hawa wote waliwahi kuitumikia CCM, ambapo Waitara aliitumikia CCM mwaka 1998 hadi mwaka 2008 wakati Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM.

Kwa mujibu wa sheria wanasiasa hawa wamejiunga katika nyadhifa zao ikiwemo ubunge walioupata mwaka 2015.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 nchini Tanzania, kumekuwa na wimbi la wanasiasa hasa wabunge na madiwani wa upinzani kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na chama tawala huku baadhi ya wabunge wa chama tawala wakihamia upinzani.

Kujiuzulu kwa wanasiasa hao kumesababisha serikali kutumia mamilioni ya fedha za walipa kodi kugharamia uchaguzi wa marudio katika maeneo mbalimbali nchini.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>