Published On: Tue, Jul 3rd, 2018
Sports | Post by jerome

JAPAN NA MEXICO YAAGA KOMBE LA DUNIA

Share This
Tags

Kocha wa Japan, AKIRA NISHINO amekiri kusikitishwa baada ya kikosi chake kuondolewa kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi, kufuatia kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Ubelgiji jana.

Amesema hakutarajia kupigo hicho, baada ya Nacer Chadli wa Ubelgiji kutia wavuni bao la ushindi katika dakika ya 94 ya mchezo huo, hivyo kuzima kabisa ndoto za Japan kuingia katika hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo.

Brazil nayo imeondoka na ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Mexico, ambayo pia imeyaaga mashindano hayo jana.

Brazil sasa itakutana na Ubelgiji kwenye mchezo unaotabiriwa kuwa utakuwa mgumu katika hatua ya robo fainali.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>