Published On: Wed, Jul 11th, 2018

IGP kutuma timu maalum kufuatilia wizi wa mifugo wilayani Butiama.

Share This
Tags

Baadhi ya Wananchi Wilayani Butiama Mkoani Mara wamelalamikia vitendo vya Wizi wa mifugo vinavyodaiwa kufanywa na wakazi wa maeneo hayo huku Viongozi wa Serikali za mitaa wakiwatetea pindi wanapofikishwa katika vyombo vya Dola.

Hayo yamebainishwa mbele ya  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro na Uongozi wa Polisi mkoa wa Mara alipokuwa akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Kiabakari ikiwa ni muendelezo wa ziara yake inayoendelea katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzipatia ufumbuzi wa haraka ili wananchi waendelee kufanya kazi zao kwa Amani na utulivu.

Kufuatia hali hiyo IGP Sirro  amekemea vitendo hivyo ambapo pia amesema atapeleka timu maalum ya kushughulika na suala hilo ili kulifanyia kazi.

IGP anaendelea na ziara yake huku akitumia usafiri wa Helkopta ili kujionea kwa uhalisia maeneo hayo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto za uhalifu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>