Published On: Tue, Jul 3rd, 2018
Sports / World | Post by jerome

HATIMAYE VIJANA 12 WALIOKUWA WAMEKWAMA KWENYE TUNDU LA TOPE WAMEPATIKANA THAILAND

Share This
Tags

Timu ya soka ya vijana 12 pamoja na kocha wao walionasa kwenye pango lililojaa maji kutokana na mafuriko kwa siku tisa, hatimaye wamepatikana wakiwa wa afya, baada ya msako mgumu uliofanywa na wataalamu wa kuogelea ambao hatimaye walifanikiwa kuwaona vijana hao waliokwama kwenye tundu lenye tope.

Hakukuwa na mawasiliano na vijana hao walio na umri wa kati ya miaka 11 na 16, tangu walipopotea wakiwa na kocha wao mwenye miaka 25, mnamo Juni 23.

Juhudi kubwa zilizofanywa na waokozi wa kimataifa kwa siku kadhaa zilizuiwa na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika pango hilo la Tham Luang, kaskazini mwa Thailand, na kuzuia uwezekano wa kufikiwa kwa eneo ambalo vijana hao walidhaniwa kuwepo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>