Published On: Wed, Jul 25th, 2018
Sports | Post by jerome

FIFA yataja watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia: Kylian Mbappe, Kevin De Bruyne, Eden Hazard, Cristiano Ronaldo, Mo Salah, Lionel Messi

Share This
Tags

Mchezaji kinda Mfaransa Kylian Mbappe na Mwingereza Harry Kane ni miongoni mwa wachezaji walioorodheshwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2018.

Eden Hazard wa Chelsea, Mohamed Salah kutoka Liverpool, Kevin De Bruyne wa Manchester City na mshambuliaji mpya wa Juventus Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa waliojumuishwa.

Lucy Bronze kutoka Uingereza pia amejumuishwa katika tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane mwenye miaka 24 alishinda kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka mfungaji bora katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi akiwa na magoli 6 na kuifanya England kumaliza nafasi nzuri zaidi katika mashindano haya tokea mwaka 1990.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>