Published On: Wed, Jul 25th, 2018
Sports | Post by jerome

Eritrea na Ethiopia kucheza mechi ya kihistoria mwezi Agosti

Share This
Tags

Kwa mara ya kwanza katika historia ya soka, nchi za Eritrea na Ethiopia zinatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa na viongozi wa mataifa hayo mawili yaliyokuwa kwenye vita kali kwa kipindi cha miaka 20.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa mjini Asmara nchini Eritrea kwa ridhaa ya pande zote mbili, na hii ni baada ya viongozi wa nchi Abiy Ahmed wa Ethiopia na Isaias Afwerki wa Eritrea kusaini makubaliano ya amani Julai 9 mwaka huu, na kila moja kufanya ziara kwa mwenzake ndani ya kipindi cha wiki moja tu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>