Published On: Tue, Jul 10th, 2018
World | Post by jerome

China ina uwezo wa kuhimili hasara zinazotokana na vita ya kibiashara na Marekani

Share This
Tags

Hakuna upande wowote utakaonufaika na vita ya kibiashara, kwa hivyo katika vita kubwa zaidi ya kibiashara inayoendelea kati ya China na Marekani, pande zote mbili zitakula hasara, na China imejiandaa kukabiliana na hasara hizo.

Jana usiku msemaji wa wizara ya biashara ya China ametangaza hatua nne za kupunguza athari za mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, zikiwa ni pamoja na kufuatilia athari kwa mashirika mbalimbali, kutumia nyongeza ya mapato ya kodi katika kupunguza hasara kwa mashirika yanayoathirika na wafanyakazi wao, kuhamasisha mashirika kurekebisha muundo wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje, na kuharakisha utekelezaji wa maagizo ya Baraza la serikali kuhusu kutumia vizuri mitaji ya nje na kuongeza ubora wa maendeleo ya uchumi.

Ni dhahiri kuwa serikali ya China imechukua hatua madhubuti za kupunguza athari za vita ya kibiashara, na kuonesha uwezo mkubwa wa kudhibiti na kuhimili hasara na dhamira thabiti ya kukabiliana na vita ya kibiashara, pamoja na mtizamo wa utawala unaozingatia maslahi ya umma.

Kutokana na kuwa vita hiyo ya kibiashara imeanza muda mfupi tu, bado kuna sintofahamu nyingi, na athari zake pia zinaendelea kubadilika, hali inayoihitaji China irekebishe mara kwa mara mipango yake ya kukabiliana na vita hiyo.

Wizara ya biashara ya China imesema itaendelea kurekebisha sera zake husika, na pia inakaribisha mapendekezo na maoni kutoka kwa jamii. Inakadiriwa kuwa kutokana na maendeleo ya vita ya kibiashara kati ya China na Marekani, serikali ya China itaendelea kuufanyia mabadiliko mpango wake wa kudhibiti athari za vita hiyo, ili kupunguza hasara zake kadri iwezekanavyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>