Published On: Tue, Jul 10th, 2018

Boeing 787-8 Dreamliner ni ndege ya aina gani?

Share This
Tags

Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner ni ya ukubwa wa wastani, yenye injini mbili inayotengenezwa na kampuni ya Boeing ya Marekani.

Matumizi yake ya mafuta ni wa asilimia 20 chini cha ndege ya ukubwa sawa na huo na ndiyo ndege ya Boeing inayotumia kiwango cha chini zaidi cha mafuta.

Injini zake zimejengwa kwa njia maalumu ili kupunguza sauti ndani na pia nje ya ndege kwa hadi asilimia 60.

Madirisha yake ni makubwa kuliko ya ndege zingine za ukubwa kama huo kwa asilimia 30.

Kinyume na mfumo unatumiwa kawaida wa kufungua kuongeza au kupunguza mwangaza wa dirisha kwenye ndege, kwa ndege hii nii kiponyezo hutumika kwa kutumia teknolojia ya kabadilisha rangi ya kioo kukiwezesha kudhibiti mwanangaza unaoingia.

Ina uwezo wa kubeba hadi abiria 262 ikiwa pia na uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 13,621 bila kusimama.

Boeing 787-8 ilijengwa kuchukua mahala pa ndege aina za 67-200ER na 300ER.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>