Published On: Wed, Jun 13th, 2018
World | Post by jerome

Yemen: Saudi Arabia na washirika waishambulia Hodeidah

Share This
Tags

Vikosi vinanyoungwa mkono na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia vimeanzisha mashambulizi yenye lengo la kuukamata mji wa bandari wa Hodeidah ambao uko chini ya udhibiti wa waasi wa Kihouthi nchini Yemen.

Tangazo la kuanza kwa operesheni hiyo kubwa limetolewa na serikali ya Yemen inayoishi uhamishoni nchini Saudi Arabia, ikisema vikosi vya ardhini vimenza kuukomboa mji wa Hodeidah, vikisaidia na ndege pamoja na meli za kivita.

Operesheni hiyo iliyopachikwa jina la ”ushindi wa dhahabu” imeanzishwa baada ya muda wa mwisho uliotolewa na Umoja wa Falme za Kiarabu, kwa waasi wa Kihouthi kuwa wameuachia mji huo ulio kwenye Bahari ya Sham, kupita usiku wa kuamkia leo.

Bandari ya Hodeidah ni njia muhimu ya kupitishia msaada wa kibinadamu kuelekea katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya juhudi za kidiplomasia baina ya pande zinazohasimiana kujaribu kuepusha mashambulizi katika mji wa Hodeidah, kwa hofu kwamba yangekwamisha msaada wa chakula, dawa na mafuta kwa Wayemen wengi, ambao tayari wanakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kibinadamu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>