Published On: Wed, Jun 13th, 2018
Business | Post by jerome

Wananchi wa manispaa ya Mtwara mikindani walalamikia kupanda kwa bei za bidhaa sokoni

Share This
Tags

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitr, baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mtwara Mikindani, wamelalamikia bei ya bidhaa kuwa juu, hali ambayo inawafanya washindwe kufanya manunuzi kwa ajili ya maandalizi ya skukuu hiyo.

Clouds Tv imefika katika soko kuu la manispaa hiyo kujionea pilikapilka za wakazi hao waliofika kutafuta bidhaa mbalimbali, lakini wengi wao wamekua wakilalamikia ukali wa bei za bidhaa hizo.

Wakati wanunuzi wakitoa malalamiko juu ya bei, wafanyabiashara nao wakasikika wakilalama pia juu ya ugumu wa biashara zao kutokana na wateja kuwa wachache.

Lakini pamoja na hali ya biashara kuwa ngumu kama ilivyoezwa na wafanyabiashara hao, bado wamekuwa wavumilivu kutokana na kupokea lugha za kuudhi kutoka kwa wateja wanaokwazika na bei, na hilo linathibitishwa na mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Mtwara Hamza Licheta.

Uongozi wa soko hilo, umeendelea kusisitiza amani na utulivu kwa wafanyabiashara na wateja wao katika kipindi hiki cha kuumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuelekea sikukuu ya Eid.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>