Published On: Mon, Jun 11th, 2018

WAKULIMA WALIA NA WIZI WA VANILLA MASHAMBANI KAGERA

Share This
Tags

Baadhi ya wakulima katika mkoa wa Kagera wanaojihusisha na kilimo cha zao la Vanilla wameanza kukata tamaa ya kuendeleza kilimo cha zao hilo, kutokana na kushamiri kwa vitendo  vya wizi vinavyofanywa kwenye mashamba ya wakulima na watu wasiojulikana nyakati za usiku.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  wakulima hao NURU MUSSA na AGELESTINA GERVAS wamesema kwa sasa wanalazimika kulala nje ya nyumba zao ili kulinda vanilla wanazolima.

Kwa upande wake CHARLES KAMANDO ambaye ni meneja wa shirika la maendeleo ya wakulima (MAYAWA) ambalo hujihusisha na shughuli ya kuendeleza  zao la vanilla mkoani Kagera amesema, wizi huo umechangia kushusha soko pale bidhaa hiyo  inapopelekwa mnadani.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>