Published On: Wed, Jun 13th, 2018

Wakazi wa mkoa wa Tabora wamelalamikia huduma inayotolewa katika hosptali ya rufaa Kitete .

Share This
Tags

Wakazi wa Mkoa wa Tabora  wanaofika kupata huduma ya Afya katika Hospitali ya Rufaa Kitete, wamelalamikia kuchelewa kupata huduma ya matibabu wanapofika na wagonjwa wao hasa wagonjwa wakiwa mahututi.

Majidi  Namgongo, Iddi Malembeka na Teresia Vicent ni baadhi ya wagojwa ambao wanasema ingawa huduma inayotolewa kwa sasa ni nzuri, lakini bado wanalazimika kukaa zaidi ya masaa mawili ili kupata matibabu, jambo ambalo linaweza kusababisha wagonjwa wao kupoteza maisha.

Faraja Maputa ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Muuguzi Mkunga Gay Abuya wanakiri kupokea malalamiko hayo na kusema Tatizo lililopo ni upungufu wawatumishi.

Mkoa wa Tabora unakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wa Afya ambapo watumishi waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete ni 975 wanaohudumia wananchi Milioni 2.6.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>