Published On: Mon, Jun 11th, 2018
World | Post by jerome

WAHAMIAJI 629 HATIMAYE WAKUBALIWA KUPATA HIFADHI YA HISPANIA

Share This
Tags

Uhispania imekubali kupokea wahamiaji 629 waliokwama katika meli moja ya shirika la kihisani ya Aquarius iliyokataliwa kutia nanga nchini Italia na Malta.

Meli ya Aquarius imeruhusiwa kutia nanga katika bandari ya Valencia, pwani ya mashariki ya Uhispania.

Meli hiyo ilikua imeegeshwa katika bahari kati ya Italia na Malta.

Ni jana tu ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia Matteo Salvini aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook kwamba Malta haipokei mtu yeyote, Ufaransa inawafukuza watu mpakani, Uhispania inalinda mipaka yake kwa kutuma jeshi lake, na Italia pia meanza kusema hapana kwa biashara ya binadamu, na hawataki wahamiaji haramu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>