Published On: Tue, Jun 26th, 2018
Sports | Post by jerome

Uruguay yashinda pointi zote 9, leo ni Argentina na Nigeria

Share This
Tags

Mechi za mwisho za hatua ya makundi, za timu kutoka kundi A na kundi B zimepigwa jana kushuhudiwa wenyeji timu ya taifa ya Russia wakifungwa kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo kwa kukubali kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa Uruguay, licha ya kuwa tayari wamefuzu.

Katika mechi nyingine ambayo haikuwa na maslahi ya kufuzu hatua inayofuata, Saudi Arabia ilipata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Misri wa magoli 2-1.

Ushindani mkubwa jana, ulikuwa katika kundi B, kwa kuwa kabla ya mechi timu tatu (Ureno, Hispania na Iran) zilikuwa na uhakika wa kufuzu hatua ya 16 bora kwa mujibu wa hesabu za soka, lakini Hispania na Ureno ndizo zimefuzu baada ya matokeo ya mwisho, Hispania ilimaliza kwa sare ya magoli 2-2 na Morocco na kuifanya ijiongezee alama moja hadi kufikia 5, vilevle Ureno ikagawana pointi moja moja na Irana na kuifanya ifikishe jumla ya pointi tano, lakini Iran ikafikisha 4 kwa jumla.

Leo ni zamu ya timu kutoka makundi C na D, lakini mchuano mkali zaidi ukitazamiwa kati ya Nigeria na Argentina ambazo zote zina nafasi ya kufuzu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>