Published On: Wed, Jun 13th, 2018
Business | Post by jerome

Tanzania yatajwa kuwa na uwezo wa kulisha nchi za SADC

Share This
Tags

Imeelezwa kuwa asilimia 70% ya chakula kinacholiwa katika nchi za SADC, na nchi za Afrika Mashariki inaweza kutoka Tanzania ikiwa sekta binafsi itaamka na kutumia fursa ambazo Tanzania kama nchi imejaliwa kuwa nazo hususan katika kilimo.

Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, TIC kanda ya magharibi Inocent Kahwa, katika kikao cha kutambulisha uwepo wa kituo cha TIC, katika mkoa wa Kigoma, pamoja na kuhimiza ushirikiano kati ya kituo na watumishi wa serikali katika kuhudumia wawekezaji.

Katika kikao hicho ambacho kililenga zaidi watumishi wa serikali na TIC, Meneja huyo amewataka watumishi hao kutokuwa kikwazo kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

Nae Afisa biashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Festo Nashoni, amesema ni muhimu kutoa takwimu za fursa za uwekezaji zilizopo, ili kuvutia wawekezaji, huku akieleza maeneo ambayo Manispaa ya Kigoma Ujiji imetenga kwa ajili uwekezaji.

Mapema akifungua kikao hicho Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma, Utawala na Rasilimali watu, Danieli Machunda, ameishukuru serikali kwa uwepo wa kituo cha TIC katika mkoa wa Kigoma, kwani kitachangia kasi ya uwekezaji katika mkoa huo ambao una fursa nyingi za uwekezaji.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>