Published On: Wed, Jun 6th, 2018
Sports | Post by jerome

Tanzania kuandaa michezo ya majeshi ya polisi Afrika Mashariki

Share This
Tags

Michezo ya pili ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games 2018) inatarajia kutimua vumbi jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6 mpaka 12 mwaka huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  ambapo nchi 14 tayari zimethibitisha kushiriki.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Maandalizi ya Michezo hiyo, Mkuu wa Utawala ndani ya Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Leonard Paul amesema lengo la michezo hiyo kuimarisha ushirikiano na kubadilishana mbinu za kupambana na uhalifu kupitia michezo.

Kwa upande wake Msaidizi wa Inspekta Jenerali wa Polisi Kenya, Munyi Sospeter amesema watashiriki michezo hiyo ili kuleta ushindani kwa nchi wanachama wa EAPCCO.

Mwaka jana michezo hiyo ilifanyika Kampala Uganda na Polisi Tanzania walishika nafasi ya tatu katika ushindi wa jumla na nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mwenyeji Uganda na ya pili ilikwenda Kenya.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>