Published On: Wed, Jun 13th, 2018
Featured | Post by jerome

Siku ya Eid El-fitr huamuliwa vipi?

Share This
Tags

Siku ya kwanza ya Eid El Fitr inatarajiwa kuwa siku ya Ijumaa, kulingana na kituo cha kimataifa cha maswala ya angani IAC katika mataifa mengi ya Kiislamu ikiwemo Saudia , Algeria, Libya, Misri, Kuwait na Qatar.

Tangazo hilo rasmi linategemea kuonekana kwa mwezi , iwapo mwezi utaonekana tarehe 14 mwezi Juni, mwezi mtukufu wa Ramadhan utakamilika siku ya Alhamisi, na Ijumaa itakuwa siku ya kwanza ya Eid.

Shirika hilo la IAC linatarajia kwamba mwezi utaonekana katika mataifa yote ya Kiislamu kwa kuonekana kwa macho ama kupitia darubini usiku wa tarehe 14 mwezi Juni.

Tangazo rasmi la siku kuu ya Eid hufanyika saa mbili baada ya jua kuzama kwa sababu mwezi mpya hujitokeza wakati jua linapozama ama katika kipindi cha saa moja hivi.

Kulingana na IAC , mwaka huu , mwezi unatarajiwa kuonekana dakika 49 baada ya jua kuzama mjini Rabat, dakika 46 baada ya jua kuzama mjini Mogadishu, Khartoum, Tripoli na Algeria, dakika 45 nchini Dhibout na Tunisia, dakika 44 mjini sanaa, dakika 43 mjini cairo, dakika 42 mjini Royadh, Amman na Jerusalem, dakika 41 mjini Beirut, Doha, Damascus, manama na Abu Dhabi na dakika 40 mjini Baghdad, Kuwait na Muscat.

Kuonekana kwa mwezi kunategemea pale utakapoonekana na katika hali gani ya anga.

Kulinagana na data ya idara za hali ya anga, mwezi mwengine utaonekana siku ya Jumatano, tarehe 13 mwezi Juni lakini sio rahisi kuonekana na watu wanaoangalia kwa macho.

Mwezi utaonekana kwa mara ya kwanza siku ya alhamisi, tarehe 14 mwezi Juni kwa kutumia darubini na hilo linaweza kufanyika Kusini magharibi mwa bara Asia, India na maeneo ya kaskazini mwa mwa mashariki ya kati.

Kuonekana kwa mwezi kwa kutumia macho kunaweza kufanyika Afrika Kusini, Afrika Kaskazini, kusini magharibi mwa Saudia na Kusini mwa Uhispania baadaye siku hiyo.

Pia unatarajiwa kuonekana katika maeneo ya Afrika ya kati , magharibi mwa Afrika, Marekani, Marekani ya kati, maeneo ya Caribbean na Kusini mwa Marekani siku hiyo hiyo.

Eid al-Fitr inamaanisha sherehe ya kukamilisha mfungo na hutamatisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadan.

Eid huwa sikukuu rasmi katika mataifa yote ya kiislamu lakini huwa kuna tofauti ya maadhimisho ya siku hiyo.

Waislamu kote ulimwenguni huanza kuadhimisha siku ya Eid kupitia maombi ambayo hufanyika muda mfupi baada ya alfajiri.

Hii hufuatiwa na utoaji wa Zakat ambayo ni nguzo moja muhimu ya kiislamu.

Kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadan ni likizo kuu ya kidini ya Eid al-Fitr, ambapo Waislamu kote duniani hukusanyika kwa sherehe za kumaliza mwezi mtukufu.

Hata hivyo wakati wa siku kuu hiyo kubwa takatifu ya kiislamu inapowadia, wengi wa waislamu bilioni 1.8 duniani huwa na matumaini kupata ishara ya kushiriki sherehe hizo.

Waislamu hufuata kalenda inayoambatana na mwezi.

Waislamu hufunga wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan na kujizuia kula chakula na kunywa kuanzia asubuhi hadi jioni.

Ikiwa mwezi huu ungefuata kalenda ya jua, watu ambao wanaishi sehemu fulani za dunia wangesherehekea Ramadan yao msimu wa joto huku wakiwa na siku ndefu ya jua, huku sehemu zingine za dunia zikiwa na vipindi vifupi vya misimu ya baridi.

Lakini ndani ya dini ya kiislamu kuna mdahalo kuhusu ni lini sherehe hizo zinastahili kuanza.

Waislamu kwenye nchi nyingi hutegemea habari kuhusu kuonekana kwa mwezi mpya badala ya kuangalia angani wao wenyewe.

Wengine hufuatilia kalenda ya mwezi, huku wengine nao wakifuatilia sayansi ya angani kutangaza kuonekana kwa mwezi mpya.

Kwa hivyo tarehe za Eid hutofautiana kote duniani, licha ya kuwepo tofauti ya siku moja au mbili hivi.

Kwa mfano mamlaka nchini Saudi Arabia, yenye waislamu wengi wa Sunni, hutangaza kumalizika mwezi wa Ramadan, kutokana na maoni ya watu ambao huona mwezi mpya.

Kisha Waislamu kwenye nchi zingine hufuata mkondo huo.

Lakini nchini Iran ambapo kuna waislamu wengi wa Shia hutegemea matangazo ya serikali.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>