Published On: Sat, Jun 30th, 2018

Shuga Shaa kufunga ndoa na mwanasesere Nigeria

Share This
Tags

Muigizaji wa Nigeria na mchekeshaji Benjamin Nwachukwu, anayejulikana na mashabiki wake kwa jina Shuga Shaa, amezua mjadala katika mji wa Lagos kwa kusema kwamba ana uhusiano na mwanasesere wa ngono kwa jina Tonto Shaa.

Mwanasesere huyo mrembo ana nywele bandia, kucha zilizotengezwa vizuri na huvalia vito pamoja na marashi ya bei ghali- na sasa pia ana gari lake.

Shuga Shaa alionekana akienda kutazama filamu ndani ya gari lake na mpenzi wake mpya.

Baadhi ya mashabiki wake walisikitishwa na kumtaja kuwa ‘mwenda wazimu’ na mtu ‘aliye na tatizo la kiakili’.

Wengine walimshabikia na kufanya naye mzaha.

Shuga Shaa amewashutumu wakosoaji wake akisema kuwa ”Tonto Shaa alitengezwa na binadamu kama wewe na mimi ,Hana uhai ndani yake”.

Aliambia idhaa ya BBC ya Igbo kwamba mamake anajua kuhusu uhusiano wake na Tonto Shaa na hajuti hata kidogo.

Amesema kuwa ana mpango wa kufunga ndoa na mwanasesere huyo.

”Tonto Shaa ni msichana na anafaa kuheshimiwa”, alisema Shuga Shaa.

”Yeye hunituliza akili yake, hakuna ugomvi, na hakuna nafasi ya kuvunjika moyo”.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>